WANADAMU SIO WATU MCHEZO MCHEZO.
Leo wakati narudi kazini nimekutana na bonge la mkasa, nikaona wacha nikumegeee mshikaji wangu wa faida ili na Wewe upate la kujifunza katika hili
Ilikuwa kimara stand ya mwendo kasi upande wa magari yaendayo mbezi Luis, kwa kawaida watu hupanga foleni wakati Wa kupanda magari hayo yaelekeayo mbezi Luis.
Wakati foleni ikiendelea kudumbukia kwenye Basi lilopaki kwa ajiri ya kuanza safari kuelekea mbezi Luis, kama tunavyoelewa hawakosekanagi watu wakudandia foleni kwa mbele. "hapo Ndipo nataka mjifunze"
Kingine Naomba muelewe vizuri ule msemo "Dawa ya moto Ni moto" huwa sio kila sehemu unakiwa applied (unatumika).
Basi baada ya mtu huyo kuonekana anadandia foleni kwa mbele ili Hali huna watu wamepanga foleni kwa nyuma na hakuna msimamizi yoyote aliye chukua hatua juu yake akatokea mmama mmoja na kuanza kutukana matusi (siyo ya nguoni) japo yalikuwa Ni matusi akiwatukana wasimamizi huku akihoji Ni kwanini hawakumchulia hatua yoyote mtu yule?
Wasimamizi wakamgeuzia kibao na kuita askari wamkamate.
Abiria warijaribu kadri ya uwezo wao kumtetea Abiria mwenzao Ila jitihada ziligonga mwamba mana hakuna aliyetaka ushaidi kituo cha police Ila zilikiwa kelele tu.
Mama yule aliombwa na askari ashuke chini lakini aligoma na hatimaye supervisor akaamuru watu washuke chini wapande gari nyingine na hapo Ndipo walipopata nafasi ya kumkamata mama huyo kinara wa matusi.
Wote waliokuwa wakimtetea walinyamaza kimya na kupanda Gary nyingine na kumuacha yule mama akiwa chini ya ulinzi wa askari.
MI SIKUULIZI UMEJIFUNZA NINI HAPO
ILA UTAJIJUA MWENYEWE
Ila mwandishi anasihi ustaarabu unaitajika kila kona ya maisha.
Wednesday, April 5, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment